MASAU BWIRE AWAPONDA SIMBA



Ofisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameibuka na kuwaponda kiaina Simba kwa kusema kuwa ushindi wa mabao 5-0 walioupata haimaanishi wana uwezo mkubwa.

Ruvu Shooting waliwakaribisha Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Simba walifanikiwa kuchukua pointi tatu, Bwire amesema bado ana amini timu yake ina uwezo wa kufanya vizuri.

"Ushindi wakati mwingine siyo uwezo ni mpango wa Mungu, kumbukeni askari wenye kila sifa ya uaskari, askari wale wa Sham waliotumwa kwenda kumkamata Elia katika Taifa la Israel walishindwa kumkamata siyo kwamba hawakuwa na uwezo bali ulikuwa ni mpango wa Mungu, Subirini kuche, tutaelewana tu," alisema.

Kabla ya mchezo Bwire alijipambanua kuwa timu yake itafanikiwa kuwashangaza mashabiki wa Simba kwa kuwapapasasquare kama kauli mbio yao inavyosema hali iliyofanya uongozi wa Simba kukaa kimya na kusubiri dakika 90 ziamue.

LihatTutupKomentar