MASAU BWIRE AFUNGUKA KUHUSU MPAPASO



Ofisa habari wa timu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa wamejipanga kuweza kuwapapasa wapinzani wao Singida United kwa ushindi wa mabao 3-0 uwanja wa Mabatini Pwani.

Ruvu Shooting wamecheza michezo tisa ligi kuu, wamefanikiwa kushinda michezo miwili na kutoa sare michezo minne na wamepoteza michezo mitatu na kuwafanya wakusanye pointi 10 wakiwa nafasi ya 13.

"Vijana wamejiandaa katika kila hali ili kuweza kuibuka na ushindi siku ya kesho dhidi ya Singida United, tunakwenda kumshughulikia mpinzani wetu ili tuweze kuhakikisha kwamba tunaweka upinzani mkubwa.

"Tunakwenda kushinda, tumetabiriwa kushinda mabao matatu kwa mujibu wa kijana wetu Abdul Ausi, ambaye ni mwanafunzi wangu na amefaulu vizuri masomo yake ametuhakikishia tunawapiga mabao 3," alisema.

LihatTutupKomentar