KADI NYEKUNDU YAMTOA POUL GODFREY MACHOZI

Kadi aliyopata mchezaji wa timu ya Yanga, Paul Godfrey imemliza kutokana na kuwa na mipango mingi ya kufanya kuisaidia timu yake, ila kwa kuwa imetokea ameipokea adhabu hiyo.

Paulo alipata kadi hiyo katika mchezo dhidi ya Lipuli uliochezwa jana Uwanja wa taifa na wakaibuka na ushindi wa bao 1-0, baada ya kumchezea rafu Miraji Adam dakika ya 84 aliyekuwa anaambaa na mpira kuelekea maeneo ya Beno Kakolanya.

"Ni sehemu ya mchezo hivyo najipanga kwa ajili ya michezo mingine kikubwa tumepata matokeo tumemaliza salama hilo ni jambo la msingi kwetu," alisema.

Paul ameaminiwa na kocha Mwinyi Zahera baada ya kupandishwa kikosi B na kufanikiwa kuonyesha uwezo wake ambao umemfanya aweze kupata namba kikosi cha kwanza .

LihatTutupKomentar