HII HAPA HALI YA MKWASSA KWA SASA




Katibu wa zamani wa klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa, anatarajia kurudi India kwa mara nyingine tena Novemba 6 kwa ajili ya kufanyiwa vipimo huku akifunguka kuwa anaendelea vizuri.

Mkwasa alifanyiwa upasuaji wa moyo mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu, baada ya kujiuzulu nafasi yake ya ukatibu Yanga kutokana na sababu za kiafya na nafasi yake kukaimiwa na Omary Kaya.

Mkwasa amesema kuwa anaendelea vizuri kiafya kwani amezingatia masharti yote aliyopewa na dokta wake ila anatarajia kwenda India tena kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

"Kwa sasa ninaendelea vizuri na hali yangu imezidi kuimarika kwani nazingatia masharti yote niliyopewa na dokta lakini pia nahudhuria kliniki kwa dokta Lwakatare ila natarajia kwenda India tena kwa ajili ya kufanyiwa check up katika hospitali ile ya mwanzo lakini kuhusu kurejea Yanga nitaangalia baada ya miezi sita kupita," alisema Mkwasa.

LihatTutupKomentar