HAWA HAPA WACHEZAJI WA YANGA WATAKAO IKOSA LIPULI FC

Inaelezwa afya ya kiungo mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib bado haijawa sawa hivyo ataukosa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Lipuli Fc.

Aidha majeruhi wa muda mrefu Juma Mahadhi na Baruani Akilimali watandelea kukosekana dimbani huku Mcongoman Papi Tshishimbi nae akiendelea kuuguza majeraha

"Kuelekea mchezo wa kesho bado tunaendelea kuwakosa wachezaji wetu,Juma Mahadhi,Ibrahim Ajibu,Pappy Tshishimbi na Baruan Akilimali wote hao bado wanasumbuliwa na majeraha," umethibitisha uongozi wa Yanga

Yanga inashuka kwenye uwanja wa Taifa kesho Jumanne saa moja usiku kuikabili Lipuli Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 12.

Vijana hao wa Mwinyi Zahera wameweka kambi Hoteli ya Nefaland kujiandaa na mchezo huo ambao kama wataibuka na ushindi waterejea kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi

Yanga imekuwa na mwenendo mzuri tangu kuanza kwa msimu huu ikiwa imeshinda michezo saba kati ya nane iliyocheza kwenye dimba la Taifa

Inashika nafasi ya tatu ikiwa imejikusanyia alama 22 nyuma ya Simba iliyo na alama 23 kwenye nafasi ya pili.

Simba imecheza michezo miwili zaidi ya Yanga huku vinara Azam Fc wenye alama 27 wakiwa wamecheza michezo mitatu zaidi

LihatTutupKomentar