KIPA MPYA YANGA FITI KWA MCHEZO WA KESHO

KIPA mpya wa Yanga, Klaus Kindoki kwa mara ya kwanza anatarajia kuanza kuichezea klabu hiyo katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Afrikan Lyon mchezo unaotarajiwa kuchezwa Jumapili katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kipa huyo yupo fiti tayari kwaajili ya kuibeba timu yake katika mchezo huo ambao ni maalum kwaajili ya maandalizi ya kujiandaa na mchezo wao wa ligi dhidi ya Stand United.
Alisema kikosi chao katika mchezo huo mbali na kuanza na kipa huyo kinatarajia kumkosa beki wao namba mbili Juma Abdul na winga Juma Mahadhi kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
"Abdul na Mahadhi bado awajarudi kuungana na wenzao wapo chini ya uangalizi wa daktari hivyo hawatakuwa miongoni mwa nyota watakaoshuka dimbani kuumana na Lyon Jumapili," alisema.
Hafidh aliongeza kuwa nyota wengine wote wako fiti kwaajili ya mchezo huo ambao wanaamini utakuwa wa ushindani kutokana na kukutana na timu ambayo nayo ndio kwanza inapambana kuhakikisha inajitengenezea nmazingira ya kufanya vizuri katika ligi baada ya kupanda daraja.
LihatTutupKomentar