Kiungo wa timu ya Taifa Stars, Himid Mao, anatarajiwa nchini kesho mchana Septemba 4 nchini tayari kuungana na kambi ya Stars.
Awali iliarifikwa kuwa Mao angeweza kuwasili leo lakini kutokana na mambo kuingiliana imebidi atue nchini kesho.
Stars wanakipiga na Uganda Septemba 8 huko Kampala kuanza safari ya kuwania tiketi ya kucheza mashindano hayo mwakani.