HAYA HAPA MAJIBU YA MOHAMED ISSA BANKA

"Majibu ya vipimo vya Mohamed Issa Banka ni siri na majibu yapo kwenye Shirikisho la soka Tanzania (TFF) sisi hatujui chochote wenye kujua ni TFF wao ndio munatakiwa kuwauliza maana ndio wanachama wa FIFA"

>Chama cha soka Zanzibar (ZFA)

"Majibu ya vipimo vya wachezaji wote wa Zanzibar waliochukuliwa November mwaka jana Kenya kwenye mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup tuliyapokea na kuyatuma kwenye chama cha Soka Zanzibar (ZFA), sisi tuliyapokea tu kwa niaba ya chama cha soka Zanzibar (ZFA)"

>Chama cha soka Tanzania (TFF)

"Sisi hatuji lolote kuhusu Mohamed Issa Banka kufungiwa na Shirikisho la soka Afrika (CAF) waulizwe klabu yake mpya ya Yanga. Tunachojua sisi (Mtibwa) baada ya mkataba wetu na Banka kuisha tulimwomba aongeze Mkataba akakataa tukamwambia sawa nenda kwa sababu Mtibwa ni chuo kikuu cha Soka Tanzania tukamuona kijana amesaini Yanga"

Thobias Kifaru
>Afisa habari wa Klabu ya Mtibwa Sugar

"Kumekuwa na sintofahamu kuhusu mchezaji wetu Mo Banka ni kweli kila mtu amekuwa anaongea lake huu ndio wakati sahihi wa kusubili kauli husika kutoka shirikisho letu la soka Tanzania (TFF) kama kuna suala la adhabu au kufungiwa kwa mchezaji wetu kwa sasa hatuwezi kuzungumza chochote"

Omary Kaaya
>Kaimu Katibu mkuu wa klabu ya Yanga

LihatTutupKomentar