BONDIA HASSAN MWAKINYO NJIA NYEUPEEE


Mfanyabiashara na bilionea kijana Afrika MO Dewji amezidi kuonesha mapenzi yake katika michezo zaidi, baada ya kuamua kumfadhili bondia Hassan Mwakinyo anayejiandaa kwa pambano October 20 nchini Ujerumani.
MO Dewji ambaye ndio muwekezaji kwenye club ya Simba ameonesha kumuunga mkono Hassan Mwakinyo kwa kuripotiwa kuwa atagharamia maandalizi ya bondia huyo kuelekea pambano lake la October 20 dhidi ya Wanik Awdijan.
Jina la Hassan Mwakinyo limekuwa juu zaidi baada ya kufanikiwa kumpiga bondia muingereza Samm Eggington kwa TKO, pambano lililofanyika Birmgham England, hivyo Mwakinyo baada ya awali kwenda katika pambano na Samm Eggington kwa kuunga unga Ujerumani ataenda akiwa na sapoti ya kutosha.
LihatTutupKomentar