ALICHO KISEMA ALIKIBA BAADA YA KUICHEZEA COASTAL UNION

Mwanamuziki wa Bongofleva Alikiba weekend hii aliichezea Coastal Union mchezo wake wa kwanza kama mchezaji rasmi wa timu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Arusha United uliyochezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Alikiba alicheza game hiyo akitokea benchi lakini Coastal Union ilifanikiwa kumaliza mchezo kwa kupata ushindi wa goli 1-0, hiyo ni hatua nzuri kwa Alikiba aliyeamua kucheza soka la ushindani kwa sasa na leo ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika maneno haya.
“Nina furaha kuanza kukifanyia kazi kitu ambacho nakihusudu sana baada ya muziki wangu, naishukuru Costal Union kwa kuniamini na kuungana na mimi kupitia brand yangu ya Mofaya Energy Drink na kunipa fursa ya kuwa sehemu ya timu”
“Naamini ushirikiano huu, utaleta mafanikio kwa Coastal Union na MofayaByAlikiba, Asanteni kwa kuniunga mkono kwenye jambo, tukutane dimbani!”
LihatTutupKomentar