YANGA KUMPELEKA SHULE CANNAVARO AKASOME

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kumpa heshima kubwa mchezaji wake mstaafu, Nadri Haroub 'Cannavaro' ambaye ataagwa rasmi Agosti 12 mwaka huu.

Cannavaro ataagwa mjini Morogoro ambapo kikosi cha Yanga kitashuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mawenzi Market inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili kupitia Radio One, Hussein Nyika, amesema mbali na kumuaga Cannavaro, Yanga ina mipango ya kumpeleka shule kusomea ukocha.

Hatua hiyo imekuja kutokana na heshima kubwa ambayo mchezaji huyo ameipa mafanikio makubwa klabu pamoja na timu ya taifa, Taifa Stars juu ya upambanaji wake ndani ya Uwanja.

Katika mchezo ambao Yanga itamuaga Cannavaro, wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya watakuwepo pamoja na wa filamu ikiwemo Wema Sepetu ambaye atacheza mchezo wa utangulizi na Yanga Princess.
Kuelekea mechi maalum ya kumuaga aliyekuwa beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro, uongozi wa klabu hiyo umesema utaistafisha jezi yake.

Cannavaro aliyekuwa akivaa jezi namba 23, jezi hiyo itapigwa STOP na haitoweza kutumika tena kutokana na kumuwekea heshima mchezaji huyo ambaye amepewa wadhiwa wa Umeneja wa Timu kwa sasa.

Kitendo hicho kitafanyika Agosti 12 ambapo Yanga itacheza mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya Mawenzi Market mjini Morogoro utakaokuwa wa kumuaga Cannavaro.

Yanga imeweka kambi mjini Morogoro ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu pamoja na maandalizi ya kukipiga na USM Alger katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Agsosti 19 mwaka huu jijini Dar

LihatTutupKomentar