WADHAMINI SIMBA YANGA WAPATA SHAVU

KAMPUNI ya SportPesa imekula shavu la maana baada ya kuteuliwa kushiriki tuzo za Discovery Sport Industry Awards 2018 zitakazotolewa Ijumaa hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Tuzo hizo zenye heshima kubwa Africa Kusini kwa upande wa michezo na ziko kwenye sehemu tatu ambazo ni kwa washiriki wanaofanya kazi kwenye sehemu zao hapa Afrika na nyingine nne zipo wazi kwa washiriki binafsi.
Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti, SportPesa Tanzania, Tarimba Abas alisema uteuzi huo unadhihirisha juhudi zinazofanywa na kampuni yao katika kuendeleza soka Afrika.
"Tuzo za mwaka huu zilianza Januari 1 hadi Desemba 2017 ambapo ndani ya kipindi hicho Everton na SportPesa zimeorodhesha kwa kampeini ya mwaka (Pan-Africa) ya Everton kuzuru Tanzania. Vile vile kuna vipengele viwili vya Best Sponsorship, Everton ndio anaongoza kipengele hicho kwa kampeini ya #EvertoninTZ."
"Everton FC ilifanya ziara Tanzania mwaka jana na washindi wa michuano ya SportPesa Super Cup 2017, Gor Mahia na Tanzania kunufaika kwenye sekta mbali mbali kama vile utalii," alisema Tarimba.
"Vile vile, mwaka jana SportPesa iliorodhesha katika tuzo za UK Business Football kwenye kipengele cha Best Brand Activation kwa kudhamini timu zinaoshiriki Ligi Kuu ya England za Everton FC na Hull City.
Pia inafanya kazi Kenya, Tanzania, Afrika Kusini na UK. Ndio kampuni ya kubashiri michezo inayoongoza Afrika."
SportPesa wameleta chachu kwa vilabu vya Tanzania baada ya kuzidhamini Simba, Yanga na Singida United walipoingia mkataba msimu uliopita.

LihatTutupKomentar