VICTOR MOSES ATANGAZA KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA



Na GODFREY MGAYA
WINGA wa Chelsea na Nigeria, Victor Moses ametangaza kustaafu soka ya kimataifa akiwa ana umri wa miaka 27 tu. 
Na hiyo ni baada ya kuichezea timu yake ya taifa, Super Eagles mechi 37 na kuifungia mabao 12, zikiwemo za kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 na 2018. 
Moses amesema katika taarifa yake ya jana kwamba; "Ningependa kutangaza kwamba baada ya kufikiria mno, nimefanya maamuzi ya kustaafu kucheza soka ya kimataifa. Nimejifunza mambo mazuri katika maisha yangu kwa kuvaa jezi ya Super Eagles na nimeacha kumbukumbu za kudumu. Hakuna kitu kisicho na mwisho, kama kuchezea Nigeria,". 
"Pamoja na hayo, nafikiri sasa ni wakati mwafaka kuondoka ili kuelekeza fikra zangu katika klabu yangu zaidi na familia yangu changa pamoja na kutoa mwanya kwa kizazi kingine ndani ya Super Eagle,".' 
Moses, ambaye pia ameshinda Kombe la Mataifa ya Afrika na Nigeria mwaka 2013, ameongeza: "Tayari nimezungumza na kocha (Gernot Rohr) kwa simu na ningependa kusema asante kwa viongozi wa NFF (Shirikisho la Soka Nigeria) na wachezaji wenzangu wote kwa ushirikiano wote walioonyesha kwangu kwa kipindi chote hicho. 
"Muhimu zaidi ningependa kusema asanteni kwenye watu wa Nigeria kwa kuniamini na kunisapoti kwa miaka yote hiyo,".'
WASIFU WA VICTOR MOSES
KLABU 

2007–2010 Crystal Palace 58 (11)
2010–2012 Wigan Athletic 74 (8)
2012– Chelsea 86 (7)
2013–2014 Liverpool (loan) 19 (1)
2014–2015 Stoke City (mkopo) 19 (3)
2015–2016 West Ham (mkopo) 21 (1)
SOKA YA KIMATAIFA
2010 England U21 1 (0) 
2012–2018 Nigeria 37 (12
LihatTutupKomentar