UCHAMBUZI WA MECHI YA SIMBA NA ASANTE KOTOKO HUU HAPA.

Mchezo ulianza vizuri katika kipindi cha kwanza huku Simba wakionekana kucheza vizuri dakika za awali za kipindi cha kwanza. Simba walionekana kushambulia kwa kasi zaidi kupitia kwa washambuliaji wao wawili Emmanuel Okwi pamoja na Meddie Kagere. Kwa upande wa wapinzani wao Asante Kotoko wao hawakuanza pambano kwa kasi kama Simba wao muda mwingi walianza pambano kwa kuonekana kuusoma mchezo kwanza kwani hawakuwa wakishambulia kwa kasi katika kipindi cha kwanza kama Simba. Kadri mechi ilivyozidi kuendelea Asante Kotoko walionekana kuzoea mchezo na kuanza kutengeneza mashambulizi ya kushitukiza kuelekea
katika lango la Simba. Umakini ulikuwa mdogo katika safu ya ushambuliaji ya Simba kwani timu ilionekana kutengeneza nafasi nyingi hasa kipindi cha kwanza lakini safu ya ulinzi ya wapinzani wao Asante Kotoko ilionekana kuimarika zaidi kuanzia golini kwa maana ya kufanikiwa kuzuia mashambulizi ambayo yalikuwa yanafanywa na klabu ya Simba. Dakika za mwisho za kipindi cha kwanza zina wagharimu Simba ambapo beki kama Erasto Nyoni anaonekana kuzidiwa maarifa na mshambuliaji wa Asante Kotoko ambaye anafanikiwa kumpokonya mpira na anafanikiwa kuingia ndani ya boksi na anafanikiwa kupiga shuti kali ambalo golikipa
Aishi Manula anashindwa kulicheza na mpira unagonga mwamba unarudi ndani na mshambuliaji wa Asante Kotoko anafanikiwa kufunga kirahisi kwa kichwa. Kipindi cha kwanza kinamalizika Asante Kotoko wanaongoza 1-0. Kipindi cha Pili kinaanza huku Simba wakionekana kuja na kasi yao ile ile waliyoanza nayo kipindi cha kwanza, lakini safu ya ulinzi ya Asante Kotoko iliendelea kucheza vyema kwa maana ya kuzuia mashambulizi ya Simba. Dakika 20 za mwisho Simba wanafanikiwa kusawazisha goli kupitia kwa Emmanuel Okwi ambaye anafanikia kuucheza vyema mpira ambao ulipigwa na beki Asante Kwasi.  Baadae kocha wa Simba
Patrick Aussem anafanya mabadiliko mawili ambapo aliamua kumtoa mshambuliaji Meddie Kagere na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Salamba ambaye badae alikuja akakosa mkwaju wa penati. Mabadiliko mengine ni ya kiungo James Kotei ambaye alitoka na nafasi yake ikachukuliwa na Hassan Dilunga ambaye mimi kwa upande wangu nadhani alikuja akaubadili mchezo hasa katika sehemu ya katikati. Dakika 90 zinaisha matokeo yanakuwa 1-1.

LihatTutupKomentar