UCHAMBUZI KUHUSU BINGWA WA LIGI KUU TANZANIA MSIMU UJAO HUU HAPA.

Na
 MOSES FRANCIS+255715878724
Mara nyingi linapokuja suala la kuwania ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara maarufu kama VPL basi lazima uvitaje vilabu vikubwa vya soka nchini ambavyo ni Simba, Yanga pamoja na Azam. Hivi ndivyo vilabu ambavyo vimekuwa vikipokezana kutwaa ubingwa linapokuja suala la kutwaa ubingwa wa ligi kuu. Mtibwa sugar ndio timu ya mwisho tofauti na Simba na Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu. Imefanya hivyo mnamo mwaka 1999 na 2000. Kwahiyo kwa takribani miaka 18 bingwa wa ligi kuu Tanzania bara amekuwa ni Simba na Yanga pamoja na klabu ya Azam ambayo ilikuja ikaingia katika kinyang'anyiro cha ubingwa wa ligi kuu
kwa siku za hivi karibuni tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2007. Kwahiyo kwa  hali hiyo inamaanisha kuwa hata msimu ujao mpya wa 2018 na 2019 bingwa wa ligi kuu itakuwa ni timu moja wapo kati ya Simba, Yanga au Azam Fc. Tukianza kuzitazama timu hizi moja baada ya nyingine katika kuzipa  nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu. Ukianza kuitazama Azam Fc wao nadhani kikosi chao kile walichokuwa wanakitumia kutwaa ubingwa wa ligi kuu pamoja na makombe mengine wamekibomoa tangu msimu wa mwaka jana. Nasema hivyo kwa sababu Azam kwa sasa haina wachezaji wake wazoefu kama kina John Raphael Bocco, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, pamoja na Aishi Manula. Hawa ni wachezaji muhimu wa zamani wa Azam ambao kwa sasa wamejiunga na Simba tangu msimu uliopita. Kwahiyo Azam Fc wamekuja na falsafa mpya ya kuwapa nafasi hasa vijana kwenye kikosi chao lakini wanahitaji muda zaidi kwa maana ya kucheza muda mrefu kwa maana ya kuelewana na hivyo kujikuta wakileta ushindani kwa maana ya kuwa katika nafasi ya kutwaa ubingwa. Azam inaenda kuanza ligi kuu ikiwa imeondokewa na mshambuliaji wao kinda Shaban Idd Chilunda ambaye ameondoka kwenda kucheza soka barani Ulaya. Kwahiyo nafasi ya Chilunda huenda itaendelea kuwagharimu
Azam kwani Chilunda amekuwa akifanya vizuri akiwa na Azam tangu msimu uliopita kwenye ligi alikuwa akifunga magoli ya kutosha. Kwahiyo kuondoka kwake huenda kukaiathiri azam kwa maana ya kupungukiwa na mtu ambaye alikuwa akifunga magoli ya kutosha. Kuhusu mshambuliaji Donald Ndombo Ngoma ambaye alisajiliwa na Azam akitokea Yanga yeye sidhani kama atakuwa yuko fiti kwa ajili ya kuanza kucheza mechi za ligi kuu akiwa na Azam kwa siku hivi karibuni kwasababu amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya goti ambayo aliyapata akiwa na klabu yake ya Yanga. Kwahiyo mimi kama mimi siwapi nafasi kubwa sana Azam ya kutwaa 
ubingwa msimu ujao kutokana na mapungufu makubwa waliyonayo kwenye kikosi chao. Kuhusu Yanga wana nafasi  pia kubwa ya kutwaa ubingwa msimu ujao. Nasema hivyo kwasababu Yanga haijauza wachezaji wake wengi ukiachana na Donald Ngoma ambaye kaenda Azam. Kuna idadi kubwa sana ya wachezaji wazoefu ambao wamecheza kwa muda mrefu wameelewana tofauti na Simba. Kwa mfano wachezaji kama Kelvin Yondan, Juma Abdul, Dante, Gadiel Michael Mbaga, Papa Tshishimbi, Amiss Tambwe, Thaban Kamusoko Ibrahim Ajibu Migomba, pamoja na Kakolanya. Hawa ni aina ya wachezaji ambao wamecheza kwa muda mrefu Yanga wameelewana. Kwahiyo
ongezeko la wachezaji wengine wapya waliosajiliwa kama kina Makambo, Kaseke, Ngasa pamoja na Feisal Toto ni wachezaji ambao baadhi yao wamecheza ligi kuu ya Tanzania wanauzoefu nayo. Kwahiyo Yanga endapo ikichanga karata zake vizuri inaweza ikazipiku Simba pamoja na Azam na hivyo ikajikuta ikitwaa ubingwa msimu ujao. Kwa upande wa Simba pia nafasi yao ya kutwaa ubingwa msimu ujao ipo kutokana na aina ya kikosi walichonacho. Simba ina kikosi kipana, kwa maana kuwa simba ina idadi kubwa ya wachezaji ambao wanacheza nafasi moja katika kiwango kinachokaribiana au kufanana. Nadhani hii ndio sababu kuibwa
iliyoifanya Simba itwae ubingwa msimu uliopita. Kwahiyo ongezeko jingine kubwa la wachezaji wengine wapya ambao wamesajiliwa na Simba katika dirisha hili wanakuja kuongeza nguvu ndani ya kikosi cha Simba. Wachezaji hao ni kama kina Adam Salamba, Marcel Kaheza, Letius Chama, Paschal Wawa, Deogratius Munishi, pamoja na Mohamed Rashid. Kwahiyo nafasi ipo kwa Simba kwa maana ya kufanikiwa kutetea ubingwa msimu ujao kutokana na aina ya wachezaji waliopo Simba kwa sasa.

LihatTutupKomentar