TFF WAMTUMIA SALAM ZA POLE KWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JOHN POMBE MAGUFULI


RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa majonzi makubwa kifo cha dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt John Pombe Magufuli Bi.Monica Joseph Magufuli aliyefariki jana Agosti 19,2018 katika Hospitali ya Bugando,Mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu.
Rais wa TFF ndugu Karia amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho cha Bi.Monica.
“Kwa niaba ya TFF natoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli,Familia,ndugu,jamaa,marafiki na wote walioguswa na msiba huu” alisema Rais wa TFF, Karia

Pole Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kufiwa na dada 

Ameongeza kuwa wakati huu familia ikiwa katika majonzi makubwa TFF inaungana na wafiwa kuomboleza kifo cha mpendwa wao na Mungu awape nguvu na subira. 
Mungu ametoa na Mungu ametwaa jina lake lihidimiwe
LihatTutupKomentar