TETESI ZA USAJIRI

Manchester United wako tayari kumuuza mchezaji wa kiungo cha kati upande wa nyuma wa Barcelona na Colombia Yerry Mina, mwenye umri wa miaka 23, baada ya kushindwa jaribio lao la kusaini mkataba na mlinzi wa Leicester City na England Harry Maguire mwenye umri wa miaka 25. (Mirror) 

Everton hawako tayari kutimiza kiwango cha £35m kilichotolewa na Barcelona cha mchezaji Mina, na badala yake watamchukua mlinzi wa Manchester United kutoka Argentina defender Marcos Rojo, mwenye umri wa miaka 28. (Goal) 

Tottenham wamejipanga kutoa £30m kwa ajili ya mchezaji wa safu ya kati wa Bournemouth Lewis Cook mwenye umri wa miaka 21, ambaye alikuwa na hodha wa timu ya England ya vijana wenye umri wa chini ya miaka -20 iliyochukua Kombe la Dunia la msimu uliopita. (Star) 

Chelsea inakabiliwa na hatari ya kumpoteza mlinda lango wa Kibelgiji Thibaut Courtois kwa uhamisho wa bila malipoikiwa watashindwa kuajiri atakayechukua nafasi yake kabla ya kufungwa kwa kipindi cha uhamisho wa wachezaji tarehe 9 Agosti. (Mail) 

Mchezaji wa safu ya kati wa Real Madrid na Croatia Mateo Kovacic, mwenye umri wa miaka 24, hatajiunga na Manchester United kwasababu hataki kucheza chini ya uongozi wa Jose Mourinho. (Marca) 

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, mwenye umri wa miaka 23, anaweza kuondoka Paris St-Germain ikiwa Ligue 1 champions itasaini mkataba na N'Golo Kante mwenye umri wa miaka 27, kutoka Chelsea. (Mundo Deportivo, via Calciomercato) 

LihatTutupKomentar