TETESI ZA USAJIRI ULAYA LEO AUG 7,2018

Manchester United wamerudi na ofa ya mwisho kwa mlinzi wa Tottenham mwenye miaka 29 raia wa Ubelgiji Toby Alderweireld. (Mirror)
Chelsea watalipa pauni milioni 89 kwa mkataba wake Jan Oblak huko Atletico Madrid kumsaini kipa huyo wa miaka 25 raia wa Slovenia, ambaye atachukua mahala pake kipa mwenye miaka 26 raia wa Ubelgiji Thibaut Courtois, ambaye anatarajiwa kujiunga na Real Madrid. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Wakati huo huo Chelsea itamsaini kipa wa Stoke raia wa England Jack Butland ikiwa Courtois ataondoka.
West Ham wanamwinda kiungo wa kati wa Fiorentina mwenye miaka 32 raia wa Colombia Carlos Sanchez ambaye alikuwa akiichezea Aston Villa. (Mirror)

Arsenal wamefungua ofa kwa mchezaji wa miaka 27, mshambuliaji raia wa England Danny Welbeck. (Evening Standard)
Kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric, 32, anataka kuondoka Real Madrid baada ya kupata ofa nzuri kutoka Inter Milan. (La Sexta - in Spanish)
Rais Lyon Jean-Michel Aulas anasema mlinzi wa Barcelona mwenye miaka 23 Yerry Mina bado anataka kuhamia klabu hiyo ya Ufaransa licha ya ripoti kuwa mchezaji huyo wa kimataiafa wa Colombia huenda akajiunga na Everton. (Liverpool Echo)
Everton wanatarajiwa kumsaini wing'a wa miaka 25 raia wa Brazil Bernard. (Daily Mail)
Manchester United wanapanga ofa kubwa kwa kiungo wa kati wa Lazio raia wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic. (Calciomercato)
Kiungo wa kati wa Real Madrid mwenye miaka 24 raia wa Costa Rica Mateo Kovacic anatakaa kufanya mozoezi na klabu akishikiza kuondoka klabu hiyo. (Marca)
Burnely bado wana mipango ya kumsaini mshambualiaji wa Stoke raia wa England Peter Crouch. (Sun)
Leicester wako kwenye mazungumzo na Dinamo Zagreb kuhusu mkataba wa pauni milioni 13 kwa beki raia wa Croatia Filip Benkovic. (Mail)
Brentford wamekataa ofa ya Leicester ya pauni milioni 15 kwa mlinzi mwenye miaka 20 wa Wales Chris Mepham. (ESPN)
Kipa wa Southampton mwenye miaka 30 ambaye ni kipa wa zamani wa England Fraser Forster ni lengo la vilabu vya Uturuki vya Besiktas na Fenerbahce. (Sun)
Kiungo wa zamani wa Arsenal mhispania Santi Cazorla, 33, amesaini mkataba wa kudumu na Villarreal kufuatia majaribio yaliyofaulu. (EFE)
Winga wa Arsenal raia wa England Reiss Nelson anarataraijiwa aupewa mkataba wa muda mrefu. (Sun)
Derby County wamewashinda Middlesbrough katika kumasaini mshambuliaji wa Ipswich wa miaka 28 Martyn Waghorn. (East Anglian Daily Times)

Everton wamefikia makubaliano na Barcelona kumsaini mlinzi wa Colombia Yerry Mina, 23, kwa pauni milioni 28.5 kwa mkataba wa miaka mitano. (Sport - in Spanish)
Everton wamewaambia Manchester United kuwa watamchukua beki ya miaka 28 raia wa England Chris Smalling au mlizni wa Sweden Victor Lindelof, 24, ikiwa klabu hizo mbili hazitaafikia makubaliano kuhusu mlinzi raia wa Argentina Marcos Rojo, 28. (Teamtalk)
Manchester United wanajiandaa kutoa ofa kwa beki wa Leicester Harry Maguire, 25, na kwamba sasa wanaweza kulipa pesa nyingi zaidi katika rekodi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Sky Sports)
Wakati huo huo Manchester United wamefanya mawasiliano na Bayern Munich kumsaini mlinzi mwenye miaka 29 mjerumani Jorome Boateng kwa kima cha pauni milioni 44.5. (Bild - in German)

LihatTutupKomentar