SINGIDA UNTD LEO WASAINI MKATABA MPYA NA KAMPUNI HII

KAMPUNI ya Sport Master leo Jumatano wameingia mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Ligi Kuu Bara Singida United.
Mkataba huo kampuni ya Sport Master itakuwa ikiwapa Singida United vifaa vyote vya michezo kwa muda wa mwaka mmoja kama mkataba unavyosema.
Mkurugenzi wa Singida Fasto Sanga alisema wameingia mkataba huo kwa ajili ya kuwa na uhakika wa kupata vifaa vya mazoezi na mechi.
Anasema Ligi Kuu haina mdhamini kwa sasa kwani maana hiyo wamepata mzamini Sport Master atawapunguzia gharama za uendeshaji wa timu.
"Thamani ya mkataba wetu huu utakuwa tukapata asilimia 60 ya mauzo ya vifaa ambavyo tutakuwa tunatumia katika timu yetu kwa msimu wote, " alisema.
"Tutapata jezi za mazoezi na mechi, viatu, mipira, na vingine vingi ambavyo tutatumia msimu huu.
"Tunaendelea kutafuta wadhamini wengine na siku si nyingi tutatangaza wadhamini wapya ambao tutaingia nao mikataba kwa ajili ya msimu ujao, " alisema Sanga.
LihatTutupKomentar