MBWANA SAMATTA AZIDI KUTESA KIMATAIFA

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayeichezea club ya KRC Genk ya Ubelgiji
Mbwana Samatta usiku wa August 23 2018 amerudi kwenye headlines baada ya kuisaidia timu yake ya KRC Genk kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Brondby If ya Denmark.
Huo ulikuwa ni mchezo kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya UEFA Europa League msimu wa 2018/2019, Samatta akicheza game hiyo kwa dakika zote 90 na amefanikiwa kuifungia KRC Genk hat-trick katika ushindi wa magoli 5-2, Samatta alifunga goli la kwanza dakika ya 38, 55 na 70 mengine yakifungwa na Leandro Trossard dakika ya 45 na 90.
Magoli ya Brondby IF yalifungwa na Hjortur Hermannsson dakika ya 47 na Kamil Wilczek dakika ya 51, leo ndio kwa mara ya kwanza Mbwana Samatta anafunga hat-trick akiwa na KRC Genk lakini ameanza vizuri katika msimu wa 2018/2019 akiichezea KRC Genk katika mashindano tofauti ya Ligi na kuwania kufuzu hatua ya makundi ya UEFA Europa League.
Mbwana Samatta sasa akiichezea KRC Genk katika game zake nne mfululizo zilizopita amefunga jumla ya magoli 7, ambapo amecheza dakika 281 na kufunga jumla ya magoli saba ambapo ni wastani wa kufunga goli moja kila baada ya dakika 40, huu ni muendelezo mzuri kwa
Samatta hususani akiwa msimu wake wa tatu na Genk na inawezekana akavivutia vilabu vikubwa zaidi kuhitaji saini yake.

LihatTutupKomentar