KOCHA MBEYA CITY ALIA NA WAAMUZI

Kocha wa Mbeya City, Ramadhan Nswanzurwimo ameshusha lawama nzito kwa kwa waamuzi wa mchezo wao wa jana Alhamisi dhidi ya Azam.
Mbeya City ililala kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi huku mshambuliaji wa timu hiyo Eliud Ambokile akikosa Penalti.
Nswanzurwimo amesema hana tatizo na matokeo waliyopata Azam lakini ameshuhsa lawama kwa mwamuzi aliochezesha mchezo huo kuwa hakutenda haki.
Alisema waamuzi wanapaswa kujua wanatakiwa kuchezesha kwa kufuata sheria 17 za soka na si kuja uwanjani wakiwa na matokeo yao.
"Wachezaji wangu walicheza kwa kiwango kikubwa mchezo dhidi ya Azam lakini mwamuzi alituvunja moyo.
"Sina tatizo na mabao ya Azam lakini hakuna kitu kinaumiza kama mnacheza mpira halafu mwamuzi anawatoa mchezoni"alisema.
Aliongeza"Tulifunga bao zuri akakataa lakini sawa alitupa penalti lakini kipa wa Azam (Razack Abalora) alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kosa alilofanya lakini nashangaa mwamuzi akampa kadi ya njano"

LihatTutupKomentar