Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF limemtangaza rasmi nyota wa zamani wa timu ya Taifa Nigeria na klabu ya Barcelona, Emmanuel Amunike kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars kwa mkataba wa miaka miwili.
Anakumbukwa zaidi kwa mabao yake mawili aliyofunga katika fainali za kombe la dunia kule nchini Marekani, Amunike ameshinda vikombe kadhaa akiwa kama mchezaji katika nchi za Nigeria na Egypt, alipokuwa akiichezea Julius Berger F.C. na Zamalek SC.
Mwaka 1994, alijiunga na Sporting Clube de Portugal, na alifanikiwa kufunga mabao 7 kwenye msimu wake wa kwanza bila kusahau bao muhimu alilowafunga S.L. Benfica kwenye dabi ya Lisbon (1–0 na kuwapa Sporting ubingwa wa kombe la Ureno mnamo mwaka 1994),
Maelezo binafsi | |||
---|---|---|---|
Majina | Emmanuel Amunike | ||
Kuzaliwa | 25 Desemba 1970 (47) | ||
Mahali | Eziobodo, Nigeria | ||
Urefu | 1.78 m (5 ft 10 in) | ||
Nafasi | Winger | ||
Maisha ya Soka | |||
Mwaka | timu | Mechi | (G) |
1990 | Concord | ||
1991 | Julius Berger | ||
1991–1994 | Zamalek | 71 | (26) |
1994–1996 | Sporting CP | 51 | (17) |
1996–2000 | Barcelona | 19 | (1) |
2000–2002 | Albacete | 17 | (1) |
2003 | Busan I’Cons | ||
2003–2004 | Al-Wehdat | ||
Timu ya taifa | |||
1993–2001 | Nigeria | 27 | (9) |
Timu alizofundisha | |||
2008 | Al Hazm (msaidizi) | ||
2008–2009 | Julius Berger | ||
2009–2011 | Ocean Boys | ||
2014–2017 | Nigeria U17 | ||
2017–2018 | Al Khartoum SC |
Mwaka 1996 mwezi wa 12 Amunike alinunuliwa na klabua ya La Liga FC Barcelona kwa ada ya $3.6 millioni. Aliichezea Barcelona mechi tatu za msimu wa kwanza baada ya kuumia goti.
Amunike aliteseka sana na goti lake mpaka pale Barça ilipomuuza mwwka 2000, na akaelekea Albacete Balompié (ya nchini Hispania iliyokuwa ligi daraja la kwanza Segunda División). Alistaafu soka akiwa na umri wa miaka 34 . Mwaka 2008, alikwenda ligi kuu Saudi kwenye klabu ya Al-Hazm akiwa anafanya kazi kama kocha msaidizi kabla hajawa skauti wa klabu kubwa duniani Manchester United.
MAFANIKIO YAKE
Vikombe na mafanikio yake | ||
---|---|---|
1x Mchezaji bora wa kiafrika | ||
1994 | ![]() | Portugal |
1x kushiriki kombe la dunia | ||
1994 | ![]() | World Cup 1994 |
1x Kombe la Afrika | ||
1994 | ![]() | Nigeria |
1x Medali ya Olimpiki | ||
95/96 | ![]() | Nigeria |
1x Amecheza Uefa | ||
1998 | ![]() | UEFA Champions League |
2x Uefa kombe la uefa | ||
96/97 | ![]() | UEFA-Cup |
95/96 | ![]() | UEFA Cup Winners` Cup |
VIKOMBE
Alizofika fainali
CAF Nations Cup 1: 2000
Tarehe 23 Decemba 2008, Amunike alirudi klabu yake ya zamani na kuwa kocha mkuu wa Julius Berger, baada ya kumaliza mafunzo ya ukocha kule ulaya
Emmanuel Amuneke alikuwa mchezaji hatari sana miaka yake. Kocha wa kidachi bwana Clemence Westerhof alimweka benchi mechi nyingi mwaka 1994 katika michuano ya Africa Cup of Nations kule Tunisia. Mechi ya fainali walikutana na wasumbufu Zambia na jamaa huyu wa zamani wa Julius Berger ya Lagos aliingia mchezo huo na akafunga mabao mawili na kuipta timu yake ya taifa ubinwa wa kombe hilo la Afrika ikiwa ni mara yao ya pili tokea taifa hilo lifanye hivyo mwaka 1980.
Baada ya kuachwa benchi sana aliongea na waandishi wa habari na kusema
“Hakuna mchezaji anayependa kuona anaozea benchi. Lakini huwa napenda sana kuheshimu mawazo ya mwalimu hata kama maamuzi hake yapo kinyume na mapenzi yangu. Na huwa naoenda kujiri kwamba ni kweli sistahili kuoewa nafasi hiyo kwa wakati huo”
Huu ni ujmbe mzuri sana kwa wachezaji wetu wa kitanzania. Haijalishi wewe unajiona una uwezo kiasi gani. Lakini hupaswi kushindana au kujibizana na mwalimu. Unapaswa kuweka maslahi ya timu mbele.