FEI TOTO AFUNGUKA CHANZO CHA KUCHELEWA KAMBINI

Kiungo mpya wa klabu ya Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto', amesema kuwa alichelewa kujiunga na kambi ya Taifa Stars baada ya kwenda kwenye msiba wa mchezaji mweziye, Said Makapu.

Toto alikuwa Zanzibar kwa ajili ya kumpa pole Makapu ambaye lifiwa na mama yake jamb ambalo lilipelekea akaondolewa kwenye msafara wa wachezaji waliosafiri kuelekea Rwanda kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports.

Kiungo huyo aliondolewa kwenye kikosi cha Stars kwa sababu alichelewa kuripoti kambini, jambo ambalo TFF imelichukulia kama utovu wa nidhamu.

Toto anakuwa katika ile orodha ya wachezaji 6 wa Simba ambao waliondolewa pia baada ya kuchelewa kambini bila kutoa taarifa ya sababu za wao kufanya hivyo.

LihatTutupKomentar