a klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesafiri kuelekea India kwa ajili ya matibabu.
Taarifa ambazo imezipata Mkomesportnews hivi punde ni kuwa, Mkwasa amesafirishwa kuelekea nchini huko kutokana na matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Kupitia akaunti ya Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, kwenye Instagram, ameandika kumtakia kheri Mkwasa katika safari yake kuelekea India kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.
Mkwasa alitangaza kuachia ngazi ya Ukatibu Mkuu hivi karibuni akieleza kuwa hawezi kuwajibika kuendelea kuitumikia Yanga ili kulinda afya yake.
Baada ya Mkwasa kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo, uongozi ulimteua Omary Kaaya kuchukua nafasi ya Mkwasa kama Kaimu Katibu Mkuu