URUSI ULINZI UPO WA KUTOSHA YAJIWEKA TAYARI

Serikali ya Urusi imeweka mikakati kuzuia na kukabiliana kwa haraka na visa vyovyote vya mashambulio ambavyo huenda vikatokea.
Moja ya tishio ni fujo za mashabiki, hasa kutokana na uhasama kati ya Urusi na England.
Kuna pia wasiwasi wa mashambulio ya kigaidi kutokana na Syria kushiriki vita Syria.
Katika kituo kikuu cha kufuatilia ulinzi Kaliningrad, kuna makundi maalum ya maafisa wa kufuatilia picha kutoka kwa kamera za CCTV.
Kuna kamera zaidi ya 700 za aina hiyo mjini humo, na nyingine 1,200 ndani ya uwanja wa Kaliningrad, ambapo England watacheza na Ubelgiji 28 Juni.
Kwa kutumia teknolojia yakutambua nyuso za watu, watu wanachunguzwa mara moja kwa kuangalia pia hazina data ya polisi kuhusu wahalifu.
Maafisa pia wamefutwa jinsi ya kujibu shambulio la kigaidi. Mfano kuna kundi maalum kwa jina Spetsnaz la maafisa wanaoweza kutumia parachuti kuruka angani na kuingia ndani ya uwanja shambulio likitokea wakati wa mechi.

LihatTutupKomentar