TFF YAANZISHA MAFUNZO YA USAJIRI

Dirisha la usajili Tanzania lilifunguliwa Juni 15,2025-2018itafungwa July 26,2018 kwa kutumia mfumo mpya wa usajili unaotambulika kama TFF FIFA CONNECT.
Baada ya Dirisha kufungwa kutakuwa na wiki moja ya pingamizi kuanzia July 27,2018 ikifuatiwa na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kukaa kupitisha usajili.
Kuanzia leo Juni 25, TFF imeanza kutoa mafunzo ya mfumo mpya wa usajili kwa klabu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Daraja la Pili.
Mafunzo hayo yanafanyika Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) jijini Dar es salaam.
Mafunzo hayo yatafikia tamati Jumatano Juni 27,2018
TFF imezitaka timu zote kuhakikisha zinahudhuria mafunzo hayo kwani hakutakuwa na nafasi nyingine ya mafunzo baadae.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku moja kwa kila Ligi yakianza na klabu za Ligi kuu leo Juni 25-2018
LihatTutupKomentar