TETESI ZA USAJIRI ULAYA

Arsenal wana nia ya kumsaini kiungo wa kati wa Borussia Dortmund mjerumani Mario Gotze, 26. Dortmund wanataka pauni milioni 18 kwa mchezaji huyo wa miaka 26 licha ya Everton na West Ham pia kummezea mate. (Mirror)
Chelsea wamekataa ofa ya pauni milioni 18 kutoka Arsenal kwa mlinzi wa Brazil David Luiz, 31. (Le 10 Sport - in French)
West Ham wanatathmini kumwinda mlinzi wa Manchester United mwenye miak 29 Chris Smalling. Meneja mpya Manuel Pellegrini amepewa bajeti ya pauni milioni 70 kununua wachezaji. (Metro)
West Ham pia wanakaribia kumsaibi mlinzi wa England Alfie Mawson, 24, na kipa wa Poland Lukasz Fabianski, 33, kutoka Swansea. Awali Swansea walikataa ofa Kutoka West Ham kwa wachazaji hao wote. (Sky Sports)
West Ham pia wametoa ofa ya pauni milioni 25 na nyongeza ya miloni 5 kwa wing'a wa Lazio raia wa Brazil Felipe Anderson, 25. (Mail)
Juventus wanapanga kumtafuta mlinzi wa Crystal Place mholanzi Patrick van Aanholt, 27, ikiwa MBrazil Alex Sandro, 27, atakamilisha mpango wa kuhamia Manchester United. (Sun)
Newcastle wanataka pauni milioni 20 kwa mashmbulaji raia wa Serbia Aleksandar Mitrovic. Mshambuliaji huyo wa miaka 23 alikaa wa mkopo huko Fulam msimu uliopita. (Sky Sports)
Rais wa Roma James James Pallotta anasema alikuwa akifanya mzaha wakati alisema kuwa kipa Mbrazil Alisson 25 huenda akahamia Real Madrid. (Goal)
Ninataka Arsenal wawe klabu bora zaidi duniani - Emery
Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere amedokeza kuwa atatoka klabua kwenye kupitia mtandao wa Instagram. Mkataba wa muingereza huyo mwenye miak 26 unakamilika mwisho wa mwezi Juni. (Telegraph)
Aston Villa wako chini ya shinikizo za kupata pauni milioni 50 kutoka kuwauza wachezaji na huenda wakawapoteza wachezaji muhimu wakiwemo kiungo wa kati wa England Jack Grealish, 22, na beki wa wales James Chester pamoja na mshambuliaji raia wa Ivory Coast Jonathan Kodjia, 28. (Telegraph)
Tottenham wameipa Aston Villa ofa ya pauni milioni 15 kwa kiungo wake wa kati Jack Grealish, lakini Chelsea, Fulham na Leicester pia wanamtaka mchezaji huyo wa maiaka 22. (Sky Sports)
Burnley wanataka kuwasaini mlinzi wa England Craig Dawson, 28, na mshambuliaji wa England Jay Rodriguez, 28, kutoka West Brom kwa pauni milioni 28 kwa pamoja. (Mail)
Arsenal wako kwenye mazungumzo na Bayern Leverkusen kumsaini kipa mjerumani Bernd Leno, 26. (Sky Sports)
Arsenal wanakaribia kutumia pauni milioni 50 kununua wachezaji wakiwemo kiungo wa kati wa Sampdoria raia wa Uruguay Lucas Torreira, 22, na beki wa Borussia Dortmund mgiriki Sokratis Papastathopoulos, 30. (Evening Standard)
Mshambuliaji wa Manchester City Mhispania Brahim Diaz, 18, anatafutwa na meneja wa West Ham Manuel Pellegrini kwa mkopo wa muda mrefu. (Sun)
LihatTutupKomentar