SABABU ZA TIMU ZA AFRIKA KUFANYA VIBAYA KOMBE LA DUNIA HIZI HAPA


Na MOSES FRANCIS 
0715878724

Michuano ya kombe la dunia inaendelea pale Urusi. Timu za afrika zimeanza kuaga mashindano hayo na zitaendelea kuaga mashindano hayo. Nilikuwa kimya kidogo kuhusu kuzungumzia nafasi ya timu za Afrika kwenye michuano hii. Sikutaka kupoteza muda wangu kwasababu soka la Afrika ni rahisi mno kutabirika. Wakati nilipokuwa sijishughulishi na timu za Afrika kwa kuzipa nafasi kwenye michuano hii kuna kundi la watanzania wenzangu wao walikuwa wana imani na timu za Afrika. Walikuwa wanakosea. Wengi wao tumekuwa tukikutana mitaani na kuulizana nafasi ya timu hizi za Afrika kwenye michuano hii na mimi nimekuwa sinaJibu la kujibu niliendelea kukaa kimya tu. Wakati Egypt wakipoteza pambano lao dhidi ya timu mwenyeji Urusi watanzania wengi walikuwa wakiumia na kusonya kwamba Egypt wamecheza chini ya kiwango. Walikuwa wanakosea. Kinachotokea pale Urusi hasa kwa timu zetu za Afrika tu ni uhalisia tu (realism) hakuna kitu kingine. Mifumo yao ya uendeshaji wa  timu zao kwa maana ya vilabu mpaka timu ya taifa ndio unazigharimu hizi timu za Afrika pale Urusi. Kwa Mfano Egypt  ligi yao ni bora sana huku kwetu Afrika ni ligi ambayo ipo katika kiwango cha kati katika viwango vya kimataifa, kwa maana hiyo ligi nyingi za ulayani bora zaidi kuliko ligi kuu ya  Egypt kwasababu ni ligi ambazo zipo katika viwango vya juu na  si vya kati kama ilivyo kwa Egypt. Kwa maana hiyo timu za Afrika kama Egypt zilipaswa ziwe na rundo la wachezaji wengi wanaotamba ligi mbali barani ulaya kama Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, au Hispania. Tatizo la Egypt walienda kwenye michuano hii wakiamini wataenda kuishangaza dunia kwa kutumia wachezaji wa ligi yao ya ndani tu. Kikosi cha Egypt kina rundo la wachezaji wengi wanaocheza Egypt ukimweka pembeni Mohamed Salah, Mohamed Elinemy, Mohamoad Trezeguet, Ramadan Sobhi pamoja na ahmed Hegazi. Wengine wote waliobaki wanachezea Al Ahly, Zamalek, Al Marsy au Raja Casablanca. Hichi ndicho kilichowaumbua Egypt kwenye michuano hii. Unapoenda kwenye michuano kama hii unahitaji kuwa na rundo la wachezaji wanaotamba Ulaya na si Afrika. Unapokuwa Ulaya kuna mifumo mingi ya soka ambayo inamjenga na kumuimarisha mchezaji na hivyo kuingia katika soka la ushindani. Misingi ya namna hii Afrika haipo na kama ipo basi ni  kwa nchi za kaskazini mwa bara la Afrika ambazo nazo bado hazijafikia viwango vya juu. Senegal wameanza vyema michuano hii kwasababu ile ile tu ya uhalisia. Kikosi chao kina wachezaji wengiwanaotamba  barani ulaya katika vilabu mbalimbali kama Napoli,  West ham, Liverpool, Rennes,  Everton. Nigeria nao wanapita katika mfumo huu huu wa Uhalisia ambao wengi hawataki kuuamini. Kikosi cha Nigeria ni laini ni kikosi ambacho  kimekosa wachezaji imara na wapambanaji walio wengi ni vijana ambao hawawezi kuamua matokeo. Kwa mfano Nigeria kwa siku za hivi karibuni Nigeria imekosa wachezaji wenye hadhi kama ya Obafen Martins, Taribo West, Jay Jay Okocha, Nwako Kanu, wachezaji ambao walikuwa wanauwezo wa kuamua matokeo kwa uwezo wa mchezo mmoja mmoja. 
LihatTutupKomentar