CECAFA WAFANYA MABADIRIKO KAGAME CUP WAONGEZA TIMU HIZI

Shirikisho la soka ukanda wa Afrika Mashariki na kati (CECAFA) limefanya mabadiliko mengine kwa kuziongeza timu za Singida United ya Tanzania na APR ya Rwanda kwenye kichuano ya Kagame Cup 2018.
Mabadiliko haya ni baada ya mabingwa wa Ethiopia St George na Yanga Sc ya Tanzania kujiondoa katika mashindano hayo, yanayotarajiwa kuanza June 29 hadi July 13 mwaka huu jijin Dar es salaam nchini Tanzania.
Timu hizo zote zilikuwa kundi C hivyo kufanya kundi hilo kubaki na timu mbili pekee za Simba Sc ya Tanzania na Dakadaha ya Somalia.
Kulingana na ratiba mpya iliyotolewa, nafasi za Yanga Sc ya Tanzania na St George ya Ethiopia katika kundi C zinachukuliwa na vilabu vya Singida United ya Tanzania na APR ya Rwanda huku Vipers FC ikipelekwa

kundi A.
Michuano hiyo itafanyika katika viwanja viwili vya Azam Complex Chamazi na uwanja wa Taifa nchini Tanzania.
Baada ya ratiba hiyo mpya Singida United na APR zinaingia moja kwa moja kundi C na kuungana na timu za Simba ya Tanzania na Dakadaha ya Somalia.
Kundi A linaundwa na timu za Azam Fc ya Tanzania, Vipers ya Uganda, JKU ya Zanzibar na Kator FC ya Sudan Kusini.

Kundi B litakuwa na timu za
Rayon Sport ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi na Ports ya Djibouti.
LihatTutupKomentar