PESA ZA SIMBA NA YANGA NI ZA KUKOMOANA TU.


Na MOSES FRANCIS
Safu ya ushambuliaji ya simba imefunga magoli 45 msimu huu. Ni safu ya ushambuliaji ambayo imefanya vizuri kwa maana ya kufunga magoli mengi ya kutosha. Yanga wao wamefunga magoli machache sana kupitia kwa Obrey Chirwa, Pius Buswita, pamoja na Juma Mahadhi. Magoli waliyofunga wanaume hawa hayafiki 30. Kwa maana hiyo mabosi wa Yanga walikuwa wanapaswa kuingia sokoni kwa lengo la kusajili washambuliaji ambao wataisaidia timu msimu ujao. Nasikia mabosi wa Yanga walienda kwa ADAM SALAMBA. Walikuwa sahihi, Salamba ni mshambuliaji ambaye angeisaidia Yanga kwa maana ya kuiongezea nguvu katika safu ya ushambuliaji ambayo imedolola msimu huu. Badala yake Simba wakatumia pesa za Mo' kwenda kumsajili Adam Salamba kwa maana ya kuwakomoa Yanga. Huu ni usajili wa mihemuko na usiotumia akili. Tangu lini Simba ilikuwa na tatizo katika safu ya ushambuliaji??. Jibu ni hapana. Walichotakiwa Simba ni kusajili mshambuliaji mmoja wa nguvu kutoka nje ya nchi. Mshambuliaji ambaye ni msumbufu kama Donald Ngoma anayelijua goli ili aje awaongezee nguvu wa kina Okwi kwa ajili ya msimu ujao hasa katika mashindano ya klabu bingwa barani Afrika lakini si kwenda kumsajili Marcel Bonaventure au Adam Salamba.
Hawa ni aina ya wachezaji ambao hawa uzoefu wowote katika michuano ya kimataifa. Wanahitaji muda zaidi. Unapoenda kucheza na Tp Mazembe, Raja Casablanca, Kaizer Chiefs au National El Ahaly unahitaji kuwa na washambuliaji wawili wenye kimo kirefu wenye nguvu na wasumbufu ambao kwa hapa Tanzania mpaka sasa bado sijaona. Adam Salamba na Musa Bonaventure ni wachezaji wa kutumia mechi za ligi kuu, kombe la mapinduzi pamoja na kombe la Azams Sports Federation. Yanga walitinga hatua ya makundi katika michuano ya kombe la shirikisho siku za hivi karibuni kwasababu walikuwa wana Donald Ndombo Ngoma. Msimu huuu
Yanga imeonekana kuchemsha katika michuano ya kimataifa kwasababu ina Obrey Chirwa ambaye si msumbufu kama Ndombo Donald Ngoma. Simba na Yanga ifike wakati zikae chini ziache kufanya usajili wa kujinga, usajili wa kukomoana, na matokeo yake zinatumia pesa nyingi kusajili wachezaji ambao hata hawahitajiki kwa muda huo. Huwa nasiki pia Yanga ilimsajili MBUYU TWITE ambaye hakuwa hata katika mipango yao. Pesa za Yusuph Manji zilitumika kumsajili Mbuyu Twite ili tu waikomoe Simba ambayo ilikuwa inakaribia kumsajili mchezaji huyo. Katika soka la kisasa ambapo soka ni biashara usajili wa namna hii ni wa kijinga
LihatTutupKomentar