HISTORIA IMEWAGHARIMU NIGERIA RUSSIA.

Na MOSES FRANCIS
+255715878724
Nigeria haipo tena kwenye mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini Russia. Imefungwa na timu ya taifa ya Argentina mabao 2-1. Ni matokeo ambayo wengi yamewauma hasa waafrika wenzangu ambao walikuwa wakiiamini Nigeria ingeweza kufika hatua inayofuata kwa maana ya hatua ya 16 bora kwa kutoka sare na Argentina au kupata pointi tatu mbele ya Lione Messi. Mpira ni mchezo wa ajabu sana wakati mashabiki wa timu ya taifa Nigeria walioko Abuja, Tandale, Singida, au Johanesburg wakiwa na matumaini na timu yao kufuzu hatua ya mtoano mara ghafla tabasamu lao liliondoka ghalfa baada ya Marcos Rojo kuipatia   Argentina bao la ushindi. Huwa kuna matukio matatu ya kihistoria ambayo huwa yanaikabili timu ya taifa ya Nigeria katika michuano hii ya kombe la dunia na leo ningependa tu niyaseme. Tukio la kwanza ni la Nigeria kushindwa kufanya vizuri katika michuano hii. Nigeria ndio timu pekee kutoka barani Afrika ambayo imeshiriki michuano hii mara nyingi zaidi lakini haijawahi kufuzu kufika hata hatua ya robo fainali. Mara nyingi timu hii imekuwa ikiishia katika hatua ya makundi au hatua ya 16 bora tu basi. Ni Senegal, Ghana pamoja na Cameroon ndio timu za Afrika zilizofanikiwa kutika hatua ya robo fainali katika  michuano hii ya kombe la dunia kwa nyakati tofauti tofauti. Tukio la pili ni la Nigeria kuendelea kupangwa kundi moja na Argentina katika michuano hii ya kombe la dunia kwa nyakati tofauti tofauti. Nigeria imewahi kupangwa kundi moja na Argentina katika michuano ya kombe la dunia za mwaka 1994, 2002, 2010, 2014, pamoja na 2018. Tukio la tatu na la kushangaza ni la Nigeria kuendelea kupoteza dhidi ya Argentina pale wanapokutana katika mechi ya makundi katika michuano hii ya kombe la dunia. Mpaka sasa Nigeria imekutana na Argentina kwenye michuano hii ya kombe la dunia mara 5 na Nigeria imefungwa michezoyote. Endapo siku ya jana Nigeria ingefanikiwa kufuzu hatua inayofuata kupitia mgongo wa Argentina basi Nigeria ingefanikiwa kuvunja rekodi ambayo ilikuwa inakera. Wakati mshambuliaji Odian Ighalo akiwa anatazamana na golikipa Franco Armani huku miguu ikitetemeka ilikuwa ni ishara kabisa kwamba Nigeria kuna historia mbaya ambayo inaishi katika timu yao. Huenda Nigeria huwa wanaifunga Argentina lakini huwa ni katika mechi za kirafiki tu lakini kwenye michuano kama hii ile historia yao mbaya huwa ina rudi na huwa ina pumua. Kuna nyakati ambazo historia huwa haziishi lakini kwa Nigeria historia yao inawahuku

LihatTutupKomentar