TETESI ZA USAJIRI BARANI ULAYA

Mshambulijai wa Liverpool Mohamed Salah anasema kuwa hataondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu. Raia huyo wa MIsri mwenye umri wa miaka 25 amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Real Madrid (Mirror)

Kiungo wa kati wa Ivory Coast Yaya Toure, 34, atakataa maombi kutoka China na mashariki ya kati kuendelea kucheza kwa kiasi kidogo cha fedha katika ligi ya Uingereza wakati atakapoondoka Manchester City mwisho wa msimu huu. (Mail)

Manchester City inaongoza katika kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Napoli Jorginho. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Itali pia anasakwa na timu sita bora za ligi ya Uingereza.. (Times)

Eric Cantona kurudi Old Trafford
Gor Mahia kucheza dhidi ya Hull City Kenya
Barcelona yawika huku Real Madrid ikilazwa
Atletico Madrid inataka kumsaini mshambuliaji Sergio Aguero kutoka Manchester City. Raia huyo mwenye umri wa miaka29- aliondoka Madrid 2011. (Mail)

Everton inaandaa dau la £25m kumnunua beki wa Newcastle na nahodha wake Jamaal Lascelles, 24. (Mirror)

Mkufunzi wa timu ya Uingereza Gareth Southgate anapima kumshirikisha beki wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, 19, na winga wa Fulham Ryan Sessegnon, 17, katika kikosi chake cha wachezaji 35 cha kombe la dunia (Telegraph)

Juventus inajiandaa kuwasilisha ombi la £15m kwa klabu ya Chelsea ili kumnunua mshambuiliaji Alvaro Morata, 25, kwa mkopo. (Express)

Liverpool inamnyatia winga wa Brazil na Bordeaux Malcom, 21. (Mail)

Klabu mpya iliopandishwa katika ligi kuu ya Uingereza Wolves imemuorodhesha wa kwanza katika usajili wake mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Andre Silva mwisho wa msimu huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anadaiwa kugharimu £33m. (Sun)

Wolves inajiandaa kuwasilisha ombi la £30m kumsajili kipa wa Sporting Rui Patricio, 30, huku mchezaji huyo wa Ureno pia akisakwa na Napoli.(Diario de Noticias, via Birmingham Mail)

Swansea huenda ikamsajili meneja mwenye umri wa mdogo kuchukua mahala pake Carlos Carvahal baada ya ukufunzi wa Brendan Rodgers na Roberto Martinez. (Telegraph)
Mshambulaji wa Bournemouth Jermain Defoe amesema kuwa yeye mchezaji mwenza wa Uingereza Wayne Rooney walikuwa wamechoshwa na kombe la dunia la 2010 World hadi wakalazimika kutazama harusi ya Rooney katika DVD. (ESPN)

Miondoko ya densi ya Winga wa Manchester City Leroy Sane wakati wa ushindi wa kombe la ligi ilimtia wasiwasi mkufunzi Pep Guardiola, ambaye alisema kuwa kuwa aliogopeshwa na kiwango cha mchezaji huyo mwenye umri wa (Manchester Evening News)

Kipa wa Manchester City Ederson ameshinda rekodi ya dunia ya Guinness kwa kupiga mpira kwa urefu wa mita 75.35 (FourFourTwo)

Kungo wa kati wa Manchester United anyestaafu Michael Carrick anasema kuwa mkufunzi Alex Ferguson alikuwa akimchezesha wakati wa mvua. (ESPN)
LihatTutupKomentar