AZAM "YANGA LAZIMA NAFASI YA PILI WATUACHIE

Azam yajipanga kuifunika Yanga
UONGOZI wa Azam FC wamesema kuwa watapambana kuhakikisha wanashinda mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Majimaji FC itakayofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, ili waweze kumaliza katika nafasi ya pili ambayo pia inawaniwa na mabingwa watetezi wa ligi
Akizungumza na mkomesportnews Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffer Idd, alisema kuwa baada ya kupoteza nafasi ya kutwaa ubingwa, sasa wanachotaka ni kuona wanalinda heshima yao kwa kumaliza kwenye nafasi ya pili msimu huu.
Idd alisema kuwa kikosi chao kitashuka uwanjani kikiwa imara na wanafurahi kuona wachezaji wao ambao walikuwa majeruhi wamepona na wanaweza kupangwa katika mechi ya leo.
"Tunataka kusaka heshima, tayari tunajua hatuna tena nafasi ya kutwaa ubingwa kwa sababu kuna timu ambayo inapointi nyingi ambazo hatuwezi kuzifikia, kilichobakia ni kuhakikisha tunashinda na kuwa kaimu bingwa, ingawa haitupi tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa," alisema Idd.
Alizitaja mechi zao nyingine zilizobakia ni dhidi ya Tanzania Prisons itakayofanyika kwenye uwanja wake wa nyumbani halafu itamaliza msimu dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa.
Aliwataja wachezaji ambao walikuwa majeruhi na walikosa mechi iliyopita ya ugenini dhidi ya Stand United kuwa ni Aggrey Morris na Aboubakar Salum 'Sure Boy'.
LihatTutupKomentar