MKEMI AKANUSHA KUJI UDURU YANGA

Baada taarifa kutoka Jangwani kueleza kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga, Salum Mkemi, ameamua kujiweka pembeni na kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya klabu hiyo, ameibuka na kukanusha.
Awali taarifa zilieleza kuwa Mkemi alifikia hatua hiyo kutokana na mashabiki wa Yanga kudai kuwa yeye ni mmoja wa wanaoihujumu Yanga ambayo inayumba kiuchumi katika miezi ya hivi karibuni.
Alipopatikana na kuulizwa, alisema: "Mimi ni staa ndiyo maana yanazungumzwa mengi kuhusu Mimi.
"Hayo maneno na hizo taarifa sijui zimetoka wapi, Mimi bado nipo Yanga na tunaendelea na maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Azam FC kwa kuwa lengo letu sasa ni kushika nafasi ya Pili katika ligi."

LihatTutupKomentar