Jioni ya leo wakati Yanga wanapoteza pambano lao dhidi ya Mtibwa sugar pale Morogoro.Jioni

Na MOSES FRANCIS
  Jioni ya leo wakati Yanga wanapoteza pambano lao dhidi ya Mtibwa sugar pale Morogoro.Jioni ya leo wakati Chelsea wanapoteza pambano lao dhidi ya Newscastle united pale St.james park.Kuna majina wawili yalinijia kichwani. Majina haya ni PATRICK VIEIRA na ROY KEANE.Niliwahi kusoma mahala kuwa kama una wachezaji wakorofi ndani ya kikosi na wanamchango mkubwa katika timu basi kocha hana budi kujifunza jinsi ya kuishi nao. Chelsea ndo mabingwa wa ligi kuu uingereza msimu uliopita, wakati wanatwaa taji hilo kwenye kapu lao la magoli palikuwepo na magoli ya DIEGO COSTA. Costa ni mchezaji mkorofi lakini anakupa kile unachokitaka uwanjani.Kocha ANTONIO CONTE hakujua kuishi na mwanaume kama huyu. Baadae akamuruhusu aondoke, na akawa ameondoka na magoli yake.Makocha kama kina           ARSENE WENGER na mwenzake SIR ALEX FERGUSON walijifunza jinsi ya kuishi na wachezaji wakorofi kama kina patrick vieira na roy keane ambao mwisho wa siku wanakupa kile unachokitaka ambacho ni matokeo.Chelsea imemaliza nje ya top four  na hili tulilitarajia kwasababu Antonio Conte alienda kwa Alvaro Morata.Huyu ni mshambuliaji raini ambae hajui kusumbuana na mabeki.Kila muda analalamika anaonewa.Diego Costa hakuwa hivyo ni mshambuliaji ambaye alikuwa anaogopwa na mabeki.Yanga ndo mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita.Yanga kwa sasa wanawakosa wachezaji ambao mwaka jana waliwapa kile ambacho walikitaka kwa maana ya ubingwa.DONALD NDOMBO NGOMA ni mchezaji msumbufu kweli kweli.Mabeki wa timu pinzani huwa wanapatwa na wakati mgumu wakati wa kumkaba.Yanga wameshindwa kuishi na wachezaji wao wasumbufu kama kina Donald Ngoma mchezaji ambaye anaweza akagoma kucheza lakini mwisho wa siku ukiongea nae vizuri anafunga magoli ya kutosha uwanjani.Wenzetu ulaya huwa wanafika wakati wanazisahau na kuziweka pembeni sheria hasa kwa wachezaji wao wakorofi ili mradi tu wana mchango mkubwa katika timu kupata matokeo.

LihatTutupKomentar