TFF yatangaza timu za Tanzania zitakazoshiriki Kagame Cup
Rais wa TFF Wallace Karia amesema kuwa Tanzania wamekubali kuandaa michuano ya Kagame ambayo inatarajiwa kuanza mwezi June mwaka huu.
Wallace Karia amesema kuwa Tanzania itawakilishwa na timu tatu ambazo ni Azam Fc kama Bingwa Mtetezi, Yanga kama Bingwa wa Tanzania na Pia kama Mwandaaji TFF imeiomba CECAFA Tanzania iongeze Timu moja ambapo Simba imeongezwa Pia.
Kwahiyo msomaji wa Kwataunit.com Tanzania Itakwakilishwa na Yanga,Azam Fc na Simba katika Michuano hiyo Itakayokuwa na Timu 16.