CHUJI AWACHANA WACHEZAJI WA YANGA

Chuji awatolea Uvivu wachezaji wasasa wa Yanga
BAADA ya Yanga kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba, kiungo wa zamani wa timu hiyo, Athuman Idd ‘Chuji’, amewachana wachezaji wa timu hiyo kwa kuwaambia kuwa hawaijui thamani ya klabu hiyo ndiyo maana wanacheza chini ya kiwango.

Wikiendi iliyopita, Simba SC  iliibuka na ushindi huo mbele ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Matokeo hayo yameifanya Simba kuusogelea zaidi ubingwa wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 62 ikiiacha Yanga nafasi ya tatu kwa tofauti ya pointi 14.
Chuji ambaye alikuwepo uwanjani hapo akishuhudia mchezo huo, amesema wachezaji wengi wa Yanga hivi sasa wamebweteka na kushindwa kuitambua thamani ya klabu hiyo ndiyo maana wamekuwa wakicheza bila ya kujituma.
Kiungo huyo mkongwe alienda mbali zaidi na kusema kuwa, ukiangalia kikosi cha sasa cha Yanga, hakizidi wachezaji watatu ambao ndiyo wanaoipigania timu hiyo kwa moyo mmoja.

“Sisi tulikuwa tunacheza hapa hatupewi mishahara miezi mitatu au minne, lakini tulikuwa hatufungwi hivi na Simba, lakini hawa wa sasa hivi wame­bweteka.
“Utakuta mchezaji alikuwa akilipwa laki mbili na sasa analipwa laki nne basi anajiachia tu, wengi wao hawajui thamani ya nembo ya Yanga. Ni wachache tu ndiyo wanaojituma ambao hawazidi watatu,” alisema Chuji.

LihatTutupKomentar