BINGWA KATI YA  LIVERPOOL NA   REAL MADRID HATABIRIKI

Na: MOSES FRANCIS
Ulilitazama pambano la ligi kuu England kati ya Chelsea na Liverpool?. Chelsea walicheza mpira wa ovyo katika safu yao ya ushambuliaji, lakini walicheza vizuri sana katika safu yao ya ulinzi. Antonio Conte aliwaacha Liverpool wauchezee mpira jinsi wajuavyo wao  lakini hakuwaruhusu Liverpool wauchezee mpira ndani ya boksi la timu yake. Chelsea walifanikiwa kuikaba Liverpool yote, hapa namaanisha walifanikiwa kuwakaba wanaume watatu ambao wameifikisha Liverpool hapo ilipo msimu huu. Watu hawa ni Mohamed Salah, Sadio Mane, na Robetho Firminho.
Walichokuwa wanakifanya Chelsea ni kushambulia kwa kushitukiza huku wakionekana kupiga mipira mirefu ya juu kuelekea kwenye kichwa cha Olivier Giroud ambaye badae aliwapa bao na timu yote ikarudi nyuma. Imekuwa ni vigumu hasa kwa msimu huu kwa Liverpool  kucheza mechi pasipo kufunga hata goli moja. Wanaweza wakapoteza mechi lakini huwa ni vigumu kukosa kufunga hata goli moja, lakini katika pambano dhidi ya Chelsea hawakufunga hata goli moja. Yamebaki masaa machache kabla ya pambano la klabu bingwa kuchezwa pale jijini kiev. Ni pambano la aina yake  ni pambano ambalo linazikutanisha timu mbili ambazo zinafanana aina ya soka wanazocheza. Liverpool na Real Madrid zote zinashambulia kwa kasi, lakini safu zao za ulinzi ni rahisi tu kupitika. Liverpool wamefunga magoli 83 katika ligi kuu uingereza na wamefungwa magoli 38. Real madrid wamefunga magoli 92 na wamefungwa magoli 42 katika ligi kuu Hispania. Mpaka hapo ina maanisha ni ngumu kutabiri ni timu gani itaruhusu mianya kwa adui. Real madrid wana Cristian Ronaldo ambaye kwa sasa hana kasi ila ni mviziaji mzuri. Liverpool wana Mohamed Salah mwenye kasi lakini wana safu ya ulinzi inayobomoka kirahisi. Mshindi wa fainali hii huenda akapatikana extra time

LihatTutupKomentar