HAJI MANARA AMPA MBINU "DISMAS TEN"

Mara Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ametuma salamu za ushindi huo kwa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten.
Katika ujumbe huo ambao ni wa ‘kijembe’, Manara amemponda Ten kuhusu staili yake ya kuandika kimafumbo huku akiwa siyo mhamasishaji mzuri kwa mashabiki wake.
Mara kadhaa Manara amekuwa siyo mtu wa kuficha hisia zake pindi anapoona kuna jambo anahitaji kuwaambia wapinzani wao hao wa jadi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika ujumbe huu…ambao umeambatana na picha kadhaa za Ten:

“Nilikuwekea akiba..nikasema ipo siku ntakujibu...
Bro ww bado sana..unatumia lugha za mafumbo ambazo haziisaidii klabu..huna hamasa na hutoi taarifa kiweledi na kwa matakwa ya sasa ya soka na soko..njoo nikupe elimu hii..jtatu iliopita ulisema Yanga lazma watashinda..haya kiko wapi?leo nimeweka picha yako na nakutag ili walau watu wakujue kdogo....
Hii ndio Simba bro...okey karibu town @dismasten”
LihatTutupKomentar