BAADA YA KARIAKOO DERBY YANGA IJIPANGE KIMATAIFA.

Gharib Mzinga

USM ALGER
(union sportive de la Medina d alger)
Timu hii ilianzishwa mwaka 1937 tarehe 5 july, Inashiriki ligi kuu Algeria, Pia wanatumia uwanja wao uitwao Omar Hamad stadium Uliopo jijini Algeris unabeba watu 17500. Rangi zao wakiwa nyumbani ni Nyekundu na ugenini nyeupe.

Timu hii asilimia kubwa ya wachezaji wake ni raia wa algeria isipokua mmoja tu. Usm alger ni bingwa wa ligi ya Algeria mwaka 2015. Licha ya hapo wameshachukua mara 6 huko awali. Mafanikio makubwa waliyoyapata katika mashindano ya kimataifa ni Kucheza fainali ya ligi ya mabingwa africa dhidi ya Tp mazembe mwaka 2015_16.

Kwa mujibu wa Database.com Usm alger ni timu ya 19 katika rank za timu bora Africa, Ya kwanza kwa Algeria, Ya 327 kwa dunia yote. Wameingia hatua ya makundi baada ya kuitoa Plateau united ya nigeria kwa kuichalaza goli 4-0 nchini algeria, mchezo wa kwanza Usm alger ilipoteza 2-1.

Katika kundi lake Hii ndio timu bora zaidi kulinganisha na nyengine. Mchezaji wao wa kuchungwa zaidi ni mshambuliaji wake Oussama Darfalou ambaye ndie anayeongoza kwa ufungaji magoli katika ligi ya algeria amefunga goli 16. Kwa sasa Usm alger inashika nafasi ya 6 katika ligi. Sifa yao kubwa ndio timu inayoongoza kwa mashabiki wake kutokaa katika viti wao husimama na kushangilia Style ambayo inaitwa Tifo.

RAYON SPORTS. (Rwanda)
Ni timu ya soka inayoshiriki ligi kuu Rwanda. Ilianzishwa Mwaka 1968, Ni miongoni mwa timu kongwe pale Rwanda. Uwanja wao wa nyumbani ni Amahaoro (amani) stadium.

Timu hii ilianzishwa mji wa Nyanza kusini mwaka 2012 ikahamia Kigali. Imeshachukua kombe la ligi kuu (Rwanda Premier League) mara 8. Kwa sasa ipo nafasi ya Pili alama 34 nyuma ya AS kigali 35. Wachezaji wa kuchungwa zaidi ni Viungo Piere kwizera, Yannick Mukunzi na mshambuliaji wake Christ Mbondi.

Kimataifa Royon sport haina mafanikio makubwa, Huwa inatoka hatua za awali (preliminary) au hatua ya pili ya CAF klab bingwa na shirikisho Caf. Msimu huu wamefanikiwa kuingia hatua ya makundi ya Shirikisho Baada ya kuitoa Costa do sol ya msumbiji, Mchezo wa kwanza ulipigwa msumbiji Rayon ikalala 2-0, mchezo wa pili Rayon ilishinda 3-0.

GOR MAHIA (KENYA)
Mwaka 1968 tarehe 17 mwezi wa 2 timu ya soka ya Gor mahia ilianzishwa rasmi. Jina la utani ni Tetemeko la Ardhi. Timu hii inatumia uwanja wa City stadium Nairobi.  Mwalimu wa Gor ni Dylan Kerr mwalimu wa zamani wa Simba sc ya tanzania.

Gormahia imeshachukua kombe la nyumbani (kenyan premier league) mara 17. Kimataifa haijafanya vizuri sana. Ila imewahi kucheza robo fainali ya klabu bingwa africa mara mbili 1969 na 1992. Imefika hatua ya makundi ya shirikisho afrika baada ya kuitoa Gor mahia kwa sheria ya goli la ugenini. Mchezo wa kwanza ulipigwa kenya Gor ilishinda 1-0, Mchezo wa pili Ulipigwa Africa kusini Superspot ilishinda 2-1.

Wachezaji wa kuchungwa kutoka Gor mahia ni Meddie Kagere, Ernest Wendo na Tuyisinge Jacques. Kwa sasa Gor mahia ndio timu kinara Nchini kenya. Ipo kundi moja na Usm alger, Rayon sports na Young Africa katika michuano ya Shirikisho Afrika......

LihatTutupKomentar