-Winga machachari Mrisho Ngassa ambaye mkatabaa wake umeisha na klabu ya Mbeya City ya Mbeya amesema Kwa sasa anajiandaa kwa nguvu zote ili msimu ujao afanye vizuri na awe mfungaji bora kwenye ligi kuu ya Tanzania VPL itakayoanza mwezi ujayo August 26
-Ngassa ambaye alisajiliwa na timu ya mbeya City kwa mkataba wa miezi sita kwenye dirisha dogo la msimu uliopita akitokea Oman mkataba wake umeisha na sasa yuko huru na tetesi zinasema Atajiunga na klabu yake ya zamani ya Yanga. Kuondoka kwa Saimon Msuva ambaye anatarajiwa kujiunga na klabu moja ya Morocco Ngassa ana nafasi kubwa ya kusajiliwa na klabu yake hiyo
-Ngassa aliyekuwepo Juzi kwenye Harusi ya beki wa Yanga Kelvin Yondani Lamada hotel Ilala Dar
alisema
"Kwa sasa Najiandaa kujifua kwenye milima ya mwanza nina uhakika msimu ujao nitafanya vizuri na kuwa mfungaji bora wa ligi kuu"
"Timu yoyote ambayo tutafikia makubaliano nitafanya kazi nayo ila Natamani Sana kujiunga na klabu yangu ambayo Naipenda klabu ya Yanga SC, nikijunga na Yanga lazima Niwe mfungaji bora "
Alisema Mrisho Ngassa mchezaji wa zamani wa , Kagera Sugar, Simba, Yanga, Azam , na Mbeya city za hapa Tanzania.
-Ngassa kuwa mfungaji bora si Jambo geni kwake alishawahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Tanzania (VPL) akiwa mchezaji wa timu ya Yanga na Azam.