LORENZO Pellegrini nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Roma inayoshiriki Serie A ameziingiza vitani Inter Milan na Juventus ambazo zinaiwinda saini yake.
Kiungo huyo anayevaa jezi namba saba mgongoni kandarasi yake na Roma inadumu mpaka msimu wa 2021/22 tayari mabosi wa Roma nao wameanza mazungumzo naye ili aongeze kandarasi nyingine.
Nyota huyo mwenye miaka 23, raia wa Italia alijiunga na Roma 2017 akitokea Klabu ya Sassuolo ambapo alicheza mechi 47 tangu msimu wa 2015/17 na alitupia mabao 9.
Kwa sasa ndani ya Roma amecheza jumla ya mechi 66 na kupachika mabao sita na timu yake ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 26.