KOCHA wa klabu ya Espanyol ya La Liga, Abelardo Fernandez amesema kuwa mpaka sasa wana watu 10 ambao wameathirika na Virusi vya Corona.
Katika wagonjwa hao 10, wachezaji nane wa kikosi cha kwanza nao wamekuwa ni kati ya watu kumi ambao wameambukizwa Virusi vya Corona.
Wachezaji nane wa kikosi cha kwanza pamoja na makocha wawili ndiyo ambao wamepata maambukizi ya Virusi vya Corona.
Kocha huyo amesema: “ Ndani ya klabu ya Espanyol tuna kesi 10 za maambukizi ya Virusi vya Corona , wachezaji nane wa kikosi cha kwanza na makocha wawili.
“Mambo ni magumu kutokana na hali halisi ya sasa na hatujui hata hatma ya ligi ikoje na hapa tulipofika hata ligi ikirejea bado hali za wachezaji hazijawa sawa na kila mtu anatamani kurudi uwanjani," amesema.