TETESI ZA SOKA

wakamnunua mshambuliaji wao wa zamani Muargentina Carlos Tevez,35, ambaye kwa sasa anachezea Boca Juniors. (Tuttosport)
Tottenham wamekubali kuiuzia Inter Milan kwa euro milioni 20 (£16.8m) kiungo wao wa kati Christian Eriksen, 27. (Sempreinter.com)
Hata hivyo, Barcelona wanataka kumsaini Eriksen ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Denmark mwezi huu wa Januari. (Sky Sports)
GETTY IMAGES
Tottenham wamekubali kumuuza Christian Eriksen kwa Inter Milan
Chelsea wamefufua mazungumzo na Lyon kuhusu usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Moussa Dembele, 23, mwezi huu endapo watamkosa Edinson Cavani, 32 kutoka Paris St-Germain's. (Sun)
Manchester United pia wanamnyatia Cavani ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, yuko tayari kujiunga na Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)
GETTY IMAGES
Pierre-Emerick Aubameyang, 30, wa Arsenal yuko tayari kujiunga na Barcelona
Manchester United bado inapania kumsajili kiungo wa kati wa Leicester James Maddison, 23. (Star)
Chelsea na Barcelona wanamng'ang'nia beki wa Grasshoppe Mswizi Alan Arigoni, 25. (Blick)
Matumaini ya Manchester United ya kumpata Bruno Fernandes yamegonga mwamba baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia bei ya £68m iliyowekwa na Sporting Lisbon kumuuza kiungo huyo wa kati wa Portugal. (Mail)
GETTY IMAGES
Matumaini Manchester United ya kumpata Bruno Fernandes kutoka Sporting Lisbon yamegonga mwamba
Liverpool wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Isco, 27, japo inadai karibu Yuro milioni 70 (£59m) kumuachilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania. (El Desmarque - in Spanish)
Inter Milan wamekataa ofa ya mkopo kutoka kwa Manchester United kumtaka kiungo wa kati wa Uruguay Matias Vecino, 28. (Sky Sports)
Newcastle wako tayari kutoa ofa ya kumnunua beki wa Tottenham, Muingereza Danny Rose, 29. (Evening Standard)
LihatTutupKomentar