Taarifa toka timu ya JKT TZ

*TAARIFA*
Kumefanyika mabadiliko ya uwanja na muda katika mchezo wetu wa ASFC baina yetu na Tukuyu Stars ambao ulikuwa uchezwe Januari 25, 2020 katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo saa kumi jioni, badala yake mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Uhuru saa nane mchana Januari 25, 2020.

Sababu za mabadiliko hayo ni uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Jamila Mutabazi
Afisa Habari JKT TZ
Januari 24, 2020
LihatTutupKomentar