AZAM FC WAAPA KUWANYOA FASIL KENEMA


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hauna mashaka na kupoteza mchezo wao wa kwanza mbele ya Fasil Kenema ya Ethiopia nafasi ya kusonga mbeke bado ipo.

Azam FC mchezo wa kwanza wakiwa ugenini walikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 wana kibarua kizito cha kupata ushindi kwenye mchezo wa nyumbani unaotarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25 uwanja wa Chamazi.

Akizungumza na mkomesportnews Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa kwa sasa kikosi kipo kambini na kinajiaanda na mchezo wake wa marudio.

“Tumepoteza mchezo wa kwanza hatujapoteza matumaini naona tuna nafasi ya kusonga mbele ukizingatia tutakuwa nyumbani.

“Ushindani kimataifa ni mkubwa, wamepata ushindi mzuri kwao si mbaya kwetu tutatumia uwanja wetu wa nyumbani kumaliza kazi na kusonga mbele kwenye michuano ya Kimataifa,” amesema.

LihatTutupKomentar