Mwandishi wa habari za michezo nchini Rwanda, Clever Kazungu, amewapa Simba nafasi ya kushinda leo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe.
Simba itakuwa nyumbani Uwanja wa Taifa kucheza dhidi ya Mazembe baada ya kupangwa kwa droo wiki kadhaa zilizopita huko Cairo, Misri kufuatia timu hizo kutinga hatua ya robo fainali.
Kazungu anaamini kuwa Simba itapata matokeo kutokana na aina ya wachezaji ambao hivi sasa kuwa na uchu wa kufanya vema.
Ameeleza anaamini uwepo wa watu kama John Bocco na Meddie Kagere ndiyo unawapa nguvu Simba ya kupata ushindi.
Aidha, Kazungu amewataka Simba kuwa makini katika safu ya ulinzi na hata ushambuliaji katika kumaliza nafasi.
Kazungu amefunguka kwa kueleza wachezaji wa Simba wamekuwa hawana utulivu wanapopata mipira ya kumalizia jambo ambalo limekuwa likisababisha wakose nafasi nyingi.