KAMBI YA TP MAZEMBE DAR NI BALAAA

Na Godfrey Mgaya        Dar es Salaam.Kikosi cha TP Mazembe kimewasili nchini jioni ya leo kikitokea Lubumbashi DR Congo na kuweka kambi yake katika Hoteli ya Serena kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba.
Mara baada ya kufika wachezaji hao walipokelewa kwa shangwe na mashabiki wao waliojitokeza uwanja wa ndege.
Baada ya msafara wa wachezaji, benchi la ufundi na viongozi kumalizika kutoka katika vyumba vya ukagazi kwenye Uwanja huo wa ndege waliingia kwenye magari na kuanza safari ya Serena hoteli.
Msafara wa TP Mazembe uliandaliwa gari maalumu na Simba, lakini hawakupanda gari hilo bali walipanda magari yao mawili madogo.
Gari ambalo walindaliwa walipanda wale mashabiki wa TP Mazembe ambal walijitokeza katika uwanja huo wa ndege.
Mashabiki waliokuwa katika gari hilo njiani walikuwa wakiimbia nyimbo za Kikongo na kupiga shangwe la aina yake.
Saa 1:42 Usiku msafara wa TP Mazembe uliwasili katika hoteli ya Serena ambapo waliandaliwa na Simba kufikia hapo.
Mwamaspoti ambalo lilifika mpaka Serena hoteli ilishuhudia wachezaji hao wakikusanyika kwa pamoja na viongozi kisha wakaanza kuongea kwa lugha ya Kikongo na Kifaransa.
Mara baada ya kumaliza maongezi hayo walipesa kadi na Wahudumu wa hoteli hiyo ambazo watatumia katika kuingialia kwenye vyumba vyao.
Baada ya hapo mchezaji mmoja mmoja alianza kuondoka huku wengine wakionekana kupiga picha na baadhi ya mshabiki
Mpaka Mwanaspoti inaondoka Serena Hoteli wachezaji wote wa TP Mazembe walikuwa katika vyumba vya hoteli hiyo huku mashabiki na baadhi ya maofisa wa timu hiyo ndio walikuwa wakionekana nje.
LihatTutupKomentar