Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kuwa hakuna atakayezuia timu yao kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Manara amefunguka kuwa katika mbio za kuwania ubingwa kuna timu zimekaa juu kwa muda lakini ni suala la muda tu kuwa watarejea katika nafasi ya kwanza.
Amesema hana shaka na ubingwa wa ligi ila wanachokiangalia hivi sasa ni kupambana kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
"Unajua suala la ubingwa msimu huu kwenda Simba ni la muda tu.
"Kufikia mwezi Aprili mwishoni tutakuwa tayari tumeshabeba kikombe bila wasiwasi wowote."
Wakati Manara akisema hayo, Simba inaenda kucheza na JKT Tanzania leo majira ya saa 10 za jioni katika Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro