Mohamed Hussein 'Tshabalala' nahodha msaidizi wa Simba, amewatazama wachezaji wa Simba namna walivyojiandaa, akamaliza kutazama na rekodi za mechi zao zilizopita akacheka kwa furaha na kusema 'hawa wetu kabisa'.
Leo Simba watakuwa Uwanja wa Jamhuri kumenyana na Mbao mchezo wa ligi wa mzunguko wa pili huku Simba wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Kirumba.
Tshabalala amesema kuwa wanatambua utakuwa ni mchezo mgumu ila watapambana kupata matokeo kwenye mchezo wa leo.
"Tulipoteza mchezo wetu wa kwanza hayo yameshapita kwa sasa tunazungumzia wakati uliopo ni muda wetu wa kupata matokeo chanya kwani tumejipanga na morali ya wachezaji ni kubwa.
"Mbinu ambazo tumepewa na kocha wetu zinatufanya tujiamini zaidi na kupambana kupata matokeo hilo linawezekana mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema Tshabalala